Kutuhusu



Blogu/Tovuti hii ni uwanja wa kushirikishana masuala mbalimbali ya kielimu. Ni jukwaa la kusoma mada na kufikiri kwa kina kuhusu mada hizo. Ni ukurasa maalumu wa kupokea ushauri na kwenda kutekeleza ushauri huo katika maeneo au nyanja mbalimbali.
Blogu/Tovuti hii inakusudiwa isomwe na mtu mmojammoja, kikundi cha watu wachache, au kikundi cha watu wengi, kutegemeana na hali au lengo la mada husika. Kutokana na ukweli huu, mada mbalimbali zinazoandikwa kwenye blogu/Tovuti hii zitaamsha itikio, mjadala, au ukosoaji wenye lengo la kuboresha mada hizi. Ni imani yetu kwamba mada hizi zikiboreka, maisha ya wasomaji wake yataboreka pia.

Maudhui ya mada: Mada zinazoandikwa kwenye blogu/tovuti hii zinahusu masuala mbalimbali ya kijamii kama vile elimu, uchumi, ndoa, utamaduni, sanaa, maadili, afya, mazingira, n.k.
Mada hizi zimefanyiwa utafiti wa kina kwa lengo la kumwelimisha au kumnufaisha msomaji. Hata mada fupi kabisa zimeandikwa kwa kuzingatia kipengele hiki.
Walengwa: Blogu/Tovuti hii inalenga watu wa aina mbalimbali: wazee kwa vijana, wake kwa waume, matajiri kwa maskini, weusi kwa weupe.
Lugha: Blogu/Tovuti hii inatumia lugha rahisi na ya kawaida kabisa, ili kila mtu aweze kusoma mada zote bila tatizo. Kutokana na ukweli huu, lugha inayotumika kwenye mada zote ni Kiswahili.
 

0 comments:

Post a Comment